Huyu Ndiye ‘Chuma Ulete’ Anayeiba Pesa Kwenye Biashara Yako Na Jinsi Ya Kumdhibiti Ili Biashara Yako Ikue.

Umeanzisha biashara yako, unauza kweli kweli, wateja ni wengi, vitu unavyouza vinatoka kwa wingi lakini kila unapokaa na kupiga hesabu za biashara huoni faida.

Huelewi hilo linatokeaje, maana unauza sana, sasa hiyo faida inapotelea wapi? Unaona uwaulize wengine ambao wamekuwa kwenye biashara ya aina hiyo au kwenye eneo hilo na wanakupa siri ambayo hukuwa unaijua.

Wanakuambia hilo eneo kuna watu wanaitwa ‘chuma ulete’, watu hao huwa wanakuja kwenye biashara yako wakijifanya ni wateja, ila wakiondoka wanabeba faida yako yote kimazingara.

Unapewa mbinu za kuwadhibiti, lakini bado hazifanyi kazi, biashara haitengenezi faida na mwisho inakufa kabisa. Na hata isipokufa inadumaa, inakuwa haikui na kukupa mafanikio. Lengo lako la kuingia kwenye biashara halifikiwi na hali hiyo inakupa msongo zaidi.

Rafiki kama umewahi kujikuta kwenye hali hiyo, unaendesha biashara ambayo unauza sana lakini faida huioni, iwe unaamini au huamini kwenye chuma ulete, leo nakwenda kukuonesha ni wapi faida ya biashara yako inapotelea.

Kitu cha kwanza kabisa unachopaswa kujua kuhusu biashara ni kwamba mauzo mengi haimaanishi unatengeneza faida, hata kama unauza bidhaa kwa bei ya juu kuliko uliyonunulia.

Ili uweze kupata faida kwenye biashara yako, lazima ujue mzunguko wa fedha kwenye biashara hiyo. Na mzunguko wa fedha kwenye biashara unahusisha vitu viwili vikubwa, FEDHA INAYOINGIA na FEDHA INAYOTOKA kwenye biashara. Huo ni msingi ambao lazima uujue kama unataka kuendesha biashara inayotengeneza faida.

Kwa kanuni fupi kabisa na ambayo ukiijua leo itakusaidia kwenye maisha yako yote ya biashara ni hii; FEDHA INAYOINGIA kwenye biashara inapaswa kuwa kubwa kuliko FEDHA INAYOTOKA.

Njia kuu ya fedha KUINGIA kwenye biashara ni MAUZO.

Njia kuu za fedha kutoka kwenye biashara ni MANUNUZI na GHARAMA za kuendesha biashara.

Sasa wengi huwa wanafanya hivi kutafuta faida, wanachukua MAUZO – MANUNUZI, kwenye karatasi wataona wametengeneza faida, ila wanaporudi kwenye droo la pesa, wanakuta hasara.

Hapo ni kwa sababu wanakuwa hawajahusisha GHARAMA ZA BIASHARA, hivyo ili upate faida kamili kwenye biashara kanuni inapaswa kuwa MAUZO – MUNUNIZI – GHARAMA ZA BIASHARA.

Kwa kanuni hii, kabla hujaweka bei ya kuuza, jua kwanza gharama za kuendesha biashara na zijumlishe kwenye bei ya kununulia na hapo ndipo unaweza kuweka kiasi cha faida unayotaka.

MANUNUZI na MAUZO vipo wazi, lakini GHARAMA ZA BIASHARA imekuwa haipo wazi kwa wengi na hapo ndipo penye chuma ulete.

Nimekuambia hapa naenda kukuonesha chuma ulete wa biashara yako na jinsi ya kumzuia asikurudishe nyuma.

Nichukue nafasi hii kukueleza kwamba CHUMA ULETE wa biashara yako ni GHARAMA ZA BIASHARA hiyo, zile gharama zote unazoingia kwenye kuendesha biashara yako ndiyo zimekuwa zinameza faida unayotegemea kupata kwenye biashara hiyo.

Dawa ya chuma ulete wa biashara yako.

Baada ya kujua chuma ulete anayetafuna faida ya biashara yako, hatua inayofuata ni kudhibiti ili asiizuie biashara yako kukua.

Na hapo ndipo unapohitaji mafunzo maalumu ya mzunguko mzima wa fedha kwenye biashara yako.

Kwenye kitabu kipya nilichotoa kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, sura ya saba ina mafunzo kuhusu MZUNGUKO WA FEDHA kwenye biashara yako.

Sura hiyo ina vipengele hivi;

1. MAUZO NA FAIDA.

2. GHARAMA MUHIMU ZA BIASHARA.

3. GHARAMA ZA KUEPUKA KWENYE BIASHARA.

4. KUJILIPA WEWE MWENYEWE.

5. HESABU ZA FEDHA NA UMUHIMU WA MHASIBU.

Vipengele hivyo vitano vitakupa maarifa na hatua za kuchukua, ambazo ukizifanyia kazi, hutakwamishwa tena na changamoto ya kukosa faida kwenye biashara yako. Utaweza kuiendesha biashara yako vizuri, utatengeneza faida kubwa na kupata mafanikio.

Pata leo nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA na upate maarifa hayo yatakayokusaidia sana kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

Uzuri ni kwamba, kwa sasa nakupa kitabu hiki kwa bei ya zawadi kwako wewe rafiki yangu, kwa kuwa tumekuwa pamoja kwa muda mrefu. Zawadi hii ni ya muda mfupi hivyo chukua hatua sasa kuipata.

Gharama ya kupata kitabu ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sasa nakupa kama zawadi wewe rafiki yangu, utalipia tsh elfu 15 (15,000/=) tu kukipata kitabu hiki. Huu ni uwekezaji mdogo sana ambao ukiufanya, utaokoa fedha na muda wako unaopoteza kwa kufanya biashara isiyo sahihi kwako.

Kama bado hujaanza biashara, kitabu kitakusaidia kupata wazo sahihi kwako. Kama tayari upo kwenye biashara, kitabu kitakusaidia kuboresha wazo unalofanyia kazi sasa liwe sahihi kwako.

Karibu ujipatie nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA leo kabla zawadi hii hajamaliza muda wake. Wasiliana na 0752 977 170 kujipatia nakala yako sasa.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Hiki ni kitabu kinachokuwezesha wewe kujua nguvu kubwa ya kutenda miujiza ambayo iko ndani yako.

Hapo ulipo sasa, tayari una nguvu kubwa sana ndani yako, ila hujaijua na wala hujaweza kuitumia.

Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, kinakupa nafasi ya kujua nguvu hiyo na jinsi unavyoweza kuitumia.

Una uwezo wa kuwa chochote unachotaka, kufanya na kupata chochote unachotaka, lakini hiyo ni kama tu utaweza kutambua na kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yako.

Hakuna ambaye amewahi kukupa siri hii unayokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki, ni siri inayokwenda kuyafungua maisha yako na hakuna chochote kitakachofichwa tena kwako.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Zawadi hii ni ya muda mfupi na inakulenga wewe rafiki yangu, ambaye umekuwa unafuatilia mafunzo haya kwa muda mrefu, hivyo chukua hatua sasa kabla zawadi hii haijamaliza muda wake, wasiliana na 0752 977 170 na mwambie unataka zawadi ya vitabu vipya viwili; ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA na UNA NGUVU YA KITENDA MIUJIZA na utapata nakala hizo.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania

Let’s block ads! (Why?)

Leave a comment